Loading...

NDOA ZA KITAPELI SASA BASI, MHESHIMIWA MAKONDA AELEZA MPANGO

Loading...

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema kuwa atakuja na mpango wa kuanzisha mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu zote za ndoa zilizopo mkoani mwake ili kupunguza utapeli wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa na wanaume kuwa wataolewa.

Makonda amesema hayo leo Jumatatu Agosti 12, 2019, Huku akieleza kuwa  kuwa mbali ya mipango hiyo, Atatumia mkutano wa SADC  unaondelea nchini Tanzania kupata uzoefu kutoka kwa nchi nyingine kufahamu namna gani wanakabiliana na utapeli wa aina hiyo.

Kituo hicho cha kuhifadhi kumbu kumbu (Kanzi Data) kitahusisha usajili wa ndoa zote ili wanaume waliooa waweze kutambulika na kuwanusuru ili wasitapeliwe na kuumizwa mioyo yao kwa mifadhahiko ya kutegemea ndoa hewa.

“Kanzidata hii itawasaidia wanawake wasitapeliwe, mtu akitaka kukuoa utaenda mtandaoni na kuangalia taarifa zake, utabaini kama ameoa au la na vilevile itawasaidia hata wanawake ambao wameolewa ili kuzuia waume zao wasioe kwa siri,” amesema RC Makonda.

Na Juma Abdul.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

NDOA ZA KITAPELI SASA BASI, MHESHIMIWA MAKONDA AELEZA MPANGO NDOA ZA KITAPELI SASA BASI, MHESHIMIWA MAKONDA AELEZA MPANGO Reviewed by Distri Music on 8/12/2019 02:42:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.