Loading...
Watoto wanaoangalia televisheni kwa zaidi ya masaa mawili kila siku wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa athma/pumu.
Uchunguzi huo umeonyesha kuwa, kuangalia televisheni kwa muda mrefu kunaleta uwezekano wa kupata athma uongezeke mara mbili kwa watoto.
Jinsi mfumo wa kupumua unavyofanya kazi wakati mtoto anapokaa tu bila kufanya chochote, hupelekea kutokea mabadiliko katika mapafu pamoja na magojwa mengine ya kupumua ikiwemo athma.
Unene wa kupita kiasi pamoja na kutokufanya mazoezi kunakosababishwa na kuangalia muda mrefu televisheni hupelekea kutokea kwa hali hiyo, Wataalamu wamesema kuwa, kuishi maisha ya kutokuwa na shughuli yoyote katika umri mdogo hupelekea kuongezeka uwezekano wa hatari ya kupata athma ukubwani.
Hivyo wamewashauri wazazi kuwashajiisha watoto wao kufuata maisha ya kawaida ya kuwa na mishughuliko na kupunguza muda wanaoutumia kuangalia TV.
Wataalamu wa Uingereza wametoa taarifa hiyo baada ya kuwafanyia uchunguzi watoto 3,000 wa nchi hiyo kuanzia wale waliozaliwa mpaka walio na miaka 11.
Athma/pumu ni ugonjwa sugu ambao mara nyingi unawapata watoto ambapo hushindwa kupumua, pumzi kuwabana, kukohoa pamoja na kubwana na kifua.

Na Ummy Zuberi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UCHUNGUZI UMEONYESHA KUWA, KUANGALIA TV KWA MUDA MREFU HULETA 'PUMU' KWA WATOTO
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
8/07/2019 07:15:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: