Loading...

Je wajua; Homa ya mafua huongeza hatari ya mshtuko wa moyo?

Loading...
Utafiti umeonyesha kwamba kuumwa na homa ya mafua yanaweza kuongeza hatari ya kupatwa na mshtuko wa mara sita zaidi kwa kipindi cha wiki.

Utafiti huo uliohusisha maelfu ya wagonjwa wa mafua, hutoa ushahidi thabiti wa uhusiano kati ya mafua na mshtuko wa moyo.

Wanasayansi waliofanya ugunduzi huo walisema ipo haja ya watu kupata chanjo ya mafua ili kuepuka kupata mshtuko wa moyo wa mara kwa mara.

Jopo la madaktari waliofanya majaribio huko nchini Canada na kupimwa watu 20,000 ambapo walikuwa tayari na homa ya mafua kati ya mwaka 2009 hadi 2014.

Katika wagonjwa hao, 332 kati yao kwa kipindi cha mwaka mmoja waligundulika wakipata mishtuko ya moyo mara kwa na huku wakiwa na maambukizi ya homa ya mafua.

Matokeo yalionyesha kwamba siku saba baada ya kugundulika wagonjwa hao wanahoma ya mafua kasi ya kupatwa na mshtuko wa moyo uliongezeka kwa mara sita zaidi.

Mwanasayansi Dk. Jeff Kwong kutoka katika  Taasisi ya Clinical Evaluate Science huko Ontario alisema: "Hatari ipo zaidi kwa wazee na waliopatwa na mshtuko wa moyo kwa mara ya kwanza."

Dk. Kwong aliongezea: "Watu wenye hatari ya magonjwa ya moyo wanapaswa kuchukua tahadhari mapema ili kwa kuepuka homa mafua kwa kusafisha mikono na kupata chanjo mapema."

Kwakuwa hupo husiano mkubwa kati ya wagonjwa wa moyo na hatari ya kupata homa ya mafua.
Je wajua; Homa ya mafua huongeza hatari ya mshtuko wa moyo? Je wajua; Homa ya mafua huongeza hatari ya mshtuko wa moyo? Reviewed by By News Reporter on 1/25/2018 10:31:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.