Loading...

Sir Elton John atangaza kustaafu mziki

Loading...
Sir Elton John - Mtunzi na Muimbaji
Sir Elton John atangaza kuwa atastaafu baada ya kutoka katika ziara yake muziki ya kimataifa atakayoifanya kwa muda wa miaka 3. Ambapo mpaka sasa anamiaka karibia 50 katika jukwaa karibia duniani kote.

Muimbaji, mpiga kinanda, na mtengenezaji nyimbo mwenye umri wa miaka 70, alisema jana kuwa "Kwasasa ninapaswa kutenga muda mwingi na watoto wangu na mume wangu pia kuliko muziki".

Na mwanae wa kiume Zachary atakuwa na miaka 10 na miaka 8 mwanae wa kike Elijah atakapomaliza kufanya ziara hiyo ya miaka 3

Alitangaza hivyo katika tamasha moja huko New York, ambapo aliketi katika kinanda akitumbuiza nyimbo ya Tiny Dancer and I'm still standing.

Hii ndio kauli aliyozungumza Sir Elton John katika tukio hilo:
Alisema; "Vipaumbele vyangu sasa ni watoto wangu, na mume wangu, na familia yangu ...Wakati huu ni sahihi kusema asanteni mashabiki zangu wote duniani, ulimwenguni, na kisha nasema kwaherini."
Sir Elton John atangaza kustaafu mziki Sir Elton John atangaza kustaafu mziki Reviewed by By News Reporter on 1/25/2018 08:58:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.