Loading...
![]() |
Kushoto Rappa Jay-Z na kulia Rais Donald Trump |
Rappa Jay-Z, aka Shawn Carter alilaani kile alichosema rais Donald Trump wa Marekani kupitia ripoti yake kile alichosema "Shithole Countries" akifananisha nchi za Afrika kama matundu ya choo, kwani kusema hivyo kutaleta chuki na kueleweka vibaya baina nchi hizo.
"Kila mtu anahisi hasira, lakini baada ya hasira hiyo inaumiza sana kwa sababu ametazama idadi ya watu kwa ujumla wake na hakueleweka kwasababu Afrika kuna baadhi ya watu wema," akiiambia mtandao wa CNN na mwakilishi wao Van John.
Rappa aliitafakari repoti hiyo iliyotoka mapema wa mwezi huu katika mkutano wa uhamiaji uliofanyika katika Ikulu ya Marekani alipokutana na Wanasheria ambapo Trump alitoa maoni yasiyofaa kuhusu nchi za Afrika na nchi nyingine kama Haiti.
Trump alidai hakusema "Nchi za Tundu la Choo" lakini alikubali lugha 'ngumu'. Wanasheria waliohudhuria walikuwa na mawazo tofauti ya kile alichosema.
Jay-Z alipendekeza kuwa maoni ya rais ni ishara ya ubaguzi ambao unaendelea nyuma ya mlango uliofungwa and alipendekeza kutafuta nafasi ya kuzungumza na hadhara ili kutatua kashfa hiyo ya ubaguzi.
"Kwasababu mara tu baada ya kufanya hivyo, wabaguzi wengine watajificha katika mashimo wasionekane" alisema rappa huyo.
Baada ya kuelezea mfano ule ulikuwa wa kiutani, Jay-Z alisema, "Donald Trump ni binadamu, pia".
"Kama kitu kimemkwaza na anaumia nacho katika kipindi chake cha utawala wake lazima akasirike na kuelezea uchungu wake kwa namna ile" rappa huyo alisema.
Jay-Z pia alizungumzia maswala kadhaa kuwawezesha wachache Marekani, ikiwa ni pamoja na swala la ukosefu wa ajira, na alinitania kwamba sidhani kama atapata mwaliko na rais Trump Ikulu.
RAPPA JAY-Z AMGEUKIA RAIS TRUMP
Reviewed by By News Reporter
on
1/28/2018 08:35:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: