Loading...
Serikali kupitia Jaji wake mkuu Prof. Ibrahim H. Juma wametangaza rasmi siku ya mahadhimisho ya siku ya sheria na wiki ya sheria.
Jaji Mkuu alitangaza na kusema: "Ndugu wananchi napenda kuwafahamisha rasmi kwamba tunahadimisha siku ya sheria tarehe 01/02/2018, na kauli mbiu ya Siku ya Sheria ni 'Matumizi ya tehama kwa kutoa haki kwa wakati na kuzingatia maadili'."
"Kabla ya siku hiyo ya sheria kutakuwa na wiki ya sheria ambayo itakuwa na siku tano kuanzia tarehe 27/01/2018 hadi 31/01/2018, na katika hii wiki ya sheria kutakuwa na shuguli mbali mbali ambazo mahakama itashiriki na wadau mbali mbali wanaohusika katika utoaji haki; watatoa huduma za sheria, watatoa elimu ya sheria na vilevile wananchi watapata fursa ya kujifunza taratibu mbali mbali katika mfumo mzima wa utoaji haki katika kipindi hiki vilevile cha wiki ya sheria mahakimu, wasajili na watumishi wengine wa mahakama watakuwa katika vituo vya mabasi, katika mikusanyiko ya watu na watatoa elimu ya sheria na vilevile wataelezea taratibu mbali mbali za uendeshaji wa kesi mahakamani."
Aliendelea akisema
"Ningependa kuchukua nafasi hii kuwaomba wananchi wote wasikose kutumia nafasi ambayo itakuwa imejitokeza katika wiki ya sheria."
"Kilele cha Siku ya Sheria itakuwa ni tarehe 01/02/2018 katika sehemu mbali mbali nchini Tanzania lakini hapa Dar es salaam Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi."
"Ningependa kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wananchi wote."
TAARIFA KWA UMMA
Reviewed by By News Reporter
on
1/26/2018 12:54:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: