Loading...

TRUMP: MAREKANI KUISHAMBULIA SYRIA KIJESHI WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA

Loading...
Rais wa Marekani,Donald Trump anatarajia kutoa uamuzi muhimu kuhusu Syria baada ya shambulizi baya la kemikali.

Rais wa Marekani Donald Trump amezungumzia kuhusu Syria baada ya matumizi ya silaha za kemikali zilizotumiwa dhidi ya raia. Rais Trump ameonesha uwezekano wa kuendeshwa operesheni  ya jeshi nchini  Syria.

Rais Trump amesema kuwa katika kipindi cha muda wa masaa 24 hadi 48 yajoa Marekani itachukuwa uamuzi muhimu kuhusu Syria. Hayo rais wa Marekani amezungumza baada ya  mazungumzo  na viongozi wa ngazi za juu wa Marekani na jeshi kuhusu tuhuma  za matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria dhidi ya raia.

Kwa mujibu wa habari,uamuzi huo unatarajia kutolewa ndani ya siku mbili.

"Jambo hili linahusiana an ubinadamu na hatuwezi kuruhusu mambo kama hayo kuendelea",alisema Trump katka ikulu ya White House.

Trump amesema kuwa uamuzi muhimu utachukuliwa iwe ni kuhusu Syria yenyewe,Iran,Urusi au wote kwa pamoja.

Hata hivyo mpaka sasa ni serikali ya Syria inayolaumiwa kuhusika na shambulizi baya la kemikali lililopelekea vifo vya watu zaidi ya 70.
Na Geofrey Okechi.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
TRUMP: MAREKANI KUISHAMBULIA SYRIA KIJESHI WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA TRUMP: MAREKANI KUISHAMBULIA SYRIA KIJESHI WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA Reviewed by By News Reporter on 4/10/2018 04:55:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.