Rais Donald Trump amesema kiongozi wa Venezuela Nicolas Maduro anaweza kuondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi kipindi hiki ambacho Marekani imeongeza mbinyo kwa kuwawekea vikwazo vipya viongozi waandamizi wa nchi hiyo ya kijamaa.
Trump alikataa kujibu maswali kuhusu iwapo upo uwezekano wa jeshi linaloongozwa na Marekani kuingilia nchi hiyo iliyokumbwa na migogoro, akisema hawezi kufafanua mbinu za kijeshi.
"Ule ni utawala ambao, kwa kweli, unaweza kuondolewa haraka na jeshi ikiwa jeshi litaamua kufanya hivyo," Trump alitoa maoni yake Jumanne pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. "Kusema kweli ile ni sehemu mbaya duniani kwa sasa."
Mapema Jumanne, utawala wa Trump uliwawekea vikwazo viongozi wanne waandamizi katika serikali ya Rais Maduro akiwemo mkewe na makamu wa rais kwa tuhuma za ufisadi.
Ikiwa ni sehemu ya hatua hizo kali, Wamarek
Loading...
ni wamezuiwa kufanya biashara na nchi hiyo na Serikali itataifisha fedha zozote nchini Marekani mali memsapu, Cilia Flores, makamu wa rais Delcy Rodriguez, waziri wa mawasiliano Jorge Rodriguez na waziri wa ulinzi Vladimir Padrino.
"Tunaendelea kuwataja watu watiifu wanaomsaidia Maduro kuimarisha udhibiti wa jeshi na Serikali wakati raia wa Venezuela wanapata shida," ilisema taarifa ya Waziri wa Fedha, Steven T. Mnuchin.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita utawala wa Trump uliwawekea vikwazo makumi ya watu akiwemo Maduro mwenyewe kwa ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Lakini mpaka sasa ilikuwa imewaacha viongozi muhimu kama Delcy Rodriguez, pamoja na Padrino aliyepata mafunzo Marekani ikiaminika kwamba wamekalia nafasi muhimu na wanaweza kuwa na jukumu muhimu katika hatua za mpito.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIS DONALD TRUMP ATISHIA KUMPINDUA MADURO
Reviewed by By News Reporter
on
9/27/2018 06:10:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: