Hali ngumu ya maisha imemfanya mwanamke kuvua nguo nje ya lango la kuingia ofisi ya Rais Uhuru Kenyatta ili kulalamika na kuhakikisha kilio chake kinasikika.
Katika picha ambayo inasambazwa kwa kasi sana mtandaoni, mama huyo yupo nje ya lango la kuingia Jumba la Harambee, huku askari wanne wakionekana kuzungumza naye.
Kulingana na mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter kwa jina Muthui Mkenya, mwanamke huyo alivua nguo zake na kubaki na chupi baada ya askari waliokuwa wakilinda langoni, kumzuia kuingia ndani ili kukutana na Uhuru.
Kulingana na ujumbe w

Loading...
ke ambao ulisomwa na wengi ulisema, mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa, alikuwa akipiga kelele akisema anataka kukutana na rais kwa sababu ya hali ngumu ya maisha na taabu katika kuwalea wanawe.
Tangu mjadala kuhusu ushuru kuanza kuvuma humu nchini, hali ya maisha kwa wengi imekuwa kizungumkuti sana hasa baada ya Uhuru kutia saini Mswada wa Fedha wa 2018, na kuhalalisha ushuru wa 8% unaotozwa bidhaa za mafuta.
Kutiwa saini kwa mswada huo kulimaanisha bei za bidhaa nyingi nchini kupanda na kufanya maisha kuwa magumu sana kwa wengi wa Wakenya.
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MWANAMKE AVUA NGUO NJE YA IKULU YA KENYA KISA UGUMU WA MAISHA
Reviewed by By News Reporter
on
9/27/2018 06:00:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: