Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Dkt. Ndumbaro ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini Mkoani Ruvuma anachukua nafasi ya Dkt. Susan Alphonce Kolimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Dkt. Mnyepe anachukua nafasi ya Prof. Adolf Mkenda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Prof. Mkenda amechukua nafasi ya Mej. Jen. Mstaafu Gaudence Milanzi ambaye amestaafu.

Loading...
br>
Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 26 Septemba, 2018 na tarehe ya kuapishwa kwao itatangazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
26 Septemba, 2018

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
TAARIFA KWA UMMA: JPM AMTEUA DKT. NDUMBARO KAMA NAIBU WAZIRI MPYA
Reviewed by By News Reporter
on
9/26/2018 11:23:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: