Loading...
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Dk. Bashiru Ally, amekamilisha ziara yake ya siku tatu mkoani Geita, huku akiweka wazi kuwa amekwazika kutokana na kitendo cha kujibiwa kupitia mitandao ya kijamii na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe.
Tangu Jumamosi, wawili hao 'wameteka' mijadala ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya Dk. Bashiru kumtaka Membe afike kwenye ofisi ya chama kujibu tuhuma zinazomkabili.
Membe anadaiwa kutumia mtandao wa kijamii wa Twitter kumjibu Dk. Bashiru akieleza kuwa ataripoti ofisini kwake, huku akiweka masharti kuwa lazima amkute katika ofisi hiyo mtu aliyesambaza taarifa alizoziita za uzushi dhidi yake kufanya kampeni za kuwania urais mwaka 2020 kupitia CCM.
Akizungumza akiwa mkoani Geita mbele ya vyombo vya habari, baada ya kikao chake na uongozi wa CCM Mkoa, Dk. Bashiru alisema anaendelea kumwomba Membe akutane naye kwa ajili ya mazungumzo.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

BASHIRU, MEMBE MOTO UPO PALE PALE
Reviewed by By News Reporter
on
12/04/2018 06:44:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: