Loading...
WATANZANIA wanakabiliwa na hatari ya kupata maradhi ikiwamo usugu wa dawa mwilini kutokana na ulaji wa nyama na mazao mengine yatokanayo na wanyama yenye masalia ya kemikali za dawa za kutibu mifugo na mimea.
Haya yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Faustine Ndugulile, baada ya kufungua mafunzo ya wachunguzi wa masalia ya dawa za mifugo zinazipatikana kwenye mazao ya wanyama jijini Dar es Salaam.
"Wafugaji wanapaswa kutumia dawa kufuata maelekezo ya wataalamu, kwa kuzingatia muda uliopangwa uishe ndipo wachinje wanyama au kukamua maziwa badala ya kuangalia kupata pesa za haraka wanatakiwa kujali afya za binadamu kwanza," alisisitiza.
Ndugulile amezitaka mamlaka husika kukabiliana na changamoto hiyo kwa kutoa elimu na kudhibiti uwapo wa bidhaa zenye masalia ya kemikali zinazoingia sokoni kwa kuwa athari zake ni kubwa japo zinaweza zisionekane kwa haraka.

Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WALAJI WA NYAMA HATARINI KUPATA MAGONJWA
Reviewed by By News Reporter
on
12/04/2018 06:29:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: