Loading...

HATIMAYE UGONJWA WA KANSA WAPATIWA UFUMBUZI

Loading...
Wanasayansi wanaofanya utafiti kuhusu saratani katika Taasisi ya Francis Crick huko London, mji mkuu wa Uingereza, wamegundua njia mpya ya matibabu kwa kuharibu seli za saratani.

Watafiti waligundua kwamba inawezekana kuimarisha ulinzi wa mwili kwa kuhamisha seli za kinga kutoka kwa mtu mwingine.

Matumaini haya kwa wagonjwa wa saratani yatatekelezwa kuanzia 2019.

Adrian Hayday, mtaalam wa immunology, amesema wanasayansi na madaktari watakuwa wakitumia "chemotherapy" kuua seli za saratani.

Hayday amesema kuwa wamefanya maendeleo mapya baada ya njia za matibabu ambazo hazikuleta mabadiliko yoyote kwenye seli za saratani kutumika mpaka miaka michache iliyopita.

"Kwa sasa tuko katika kipindi cha awali cha matibabu, lakini kuna wagonjwa ambao watapata matibabu haya kuanzia mwaka ujao.",alisema mwanasayansi huyo.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
HATIMAYE UGONJWA WA KANSA WAPATIWA UFUMBUZI HATIMAYE UGONJWA WA KANSA WAPATIWA UFUMBUZI Reviewed by By News Reporter on 12/30/2018 06:19:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.