Loading...

STAA WA FILAMU 'ANGELINA JOLIE' KUIBUKIA KWENYE SIASA

Loading...
Mwigizaji nyota wa filamu kutoka Marekani Angelina Jolie aashiria uwezekano wa yeye kujiingiza kwenye siasa.

Angelina Jolie ambaye ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika baraza kuu linalohusika na wakimbizi alikuwa akijadili mada mbalimbali kama vile siasa,mitandao ya kijamii, unyanyasaji wa kijinsia na tatizo la wakimbizi katika mahojiano BBC Today kinachorushwa na kituo cha runinga cha BBC.

Jolie aliulizwa kama amewahi kufikiria siku moja kugombea kiti cha urais wa Marekani,

"Ungeniuliza swali hilo miaka 20 iliyopita ningecheka. Kama nisemavyo siku zote kwangu mimi naenda sehemu yeyote ninapohitajika" alijibu Jolie.

Katika hali ya kushangaza Jolie alisema anaweza kufanya kazi na jeshi na vilevile na serikali, "Kwa sasa" kuhusiana na siasa atakaa kimya aliongeza Jolie.
Na Mary Mkeu.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
STAA WA FILAMU 'ANGELINA JOLIE' KUIBUKIA KWENYE SIASA STAA WA FILAMU 'ANGELINA JOLIE' KUIBUKIA KWENYE SIASA Reviewed by By News Reporter on 12/30/2018 06:41:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.