Loading...

KABURI LA FIRAUNI LENYE MIAKA ELFU 4 LAGUNDULIWA MISRI

Loading...
Nchini Misri, katika wilaya ya El-Uksur limegunduliwa kaburi la firauni linalokisiwa kuwa umri wa miaka elfu 4. 

Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na waziri wa mambo ya kale alisema kaburi hilo la firauni limegunduliwa magharibi mwa mto Nile.

Kaburi linasemwa ni la mtawa wa dini ,Thaw Rakht If ,ambaye ndio aliyehifadhi maiti ya mke wa muungu Amon ajulikanaye kama Mut.

Katika kuta za kaburi hilo kuliandikwa majina mbali mbali ya wanafamilia, pia ndani yakaburi hilokulikuwa na majeneza 2 na masanamu mawili ya kuchonga yanayotokana na  mbao.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KABURI LA FIRAUNI LENYE MIAKA ELFU 4 LAGUNDULIWA MISRI KABURI LA FIRAUNI LENYE MIAKA ELFU 4 LAGUNDULIWA MISRI Reviewed by By News Reporter on 12/04/2018 08:09:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.