Loading...

KUTANA NA NG'OMBE MKUBWA AJABU

Loading...
Ng'ombe huyo kwa jina 'Knickers' ni mkubwa zaidi kuliko ng'ombe wote anaofugwa nao pamoja. Ng'ombe huyo mnene na mzito ajabu mwenye uzani wa kilo 1400 (uzito sawa na nyati/faru) na kimo chake ni 194 sentimita (futi 6 na nchi 4).

Ng'ombe huyo ambaye hadi sasa ana miaka saba anaaminika kuwa ng'ombe mkubwa zaidi nchini Australia na bila shaka ni kati ya ng'ombe wakubwa zaidi duniani.

Ng'ombe huyo ambaye ni wa aina ya Holstein Friesian, ni mkubwa sana ukilinganisha na ng'ombe wa aina hiyo 

Knickers amehasiwa, ikiwa na maana kuwa hawezi kutungisha mbegu.

Vitabu vya rekodi duniani vinasema kuwa, Bellino- ng'ombe kutoka Italia mwenye kimo cha 202.7 sentimeta ndiye nng'ombe mrefu zaidi kuwahi kuishi.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KUTANA NA NG'OMBE MKUBWA AJABU KUTANA NA NG'OMBE MKUBWA AJABU Reviewed by By News Reporter on 12/01/2018 08:28:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.