Loading...

KUFUATIA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI - MWANASIASA AJITANGAZA HADHARANI NI MUATHIRIKA

Loading...
Mbunge mmoja wa Uingereza alijitokeza Alhamisi, Novemba 29 na kutangaza kuwa anaishi na virusi vya UKIMWI.

Mbunge huyo aliweka hayo bayana kuhusiana na maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani.

Lloyd Russel – Moyle wa chama pinzani cha Labour mwenye umri wa miaka 32 aliwaeleza wabunge wenzake kuwa alipimwa na kubainika kuwa alikuwa na virusi vya HIV alipokuwa na umri wa miaka 22.

Moylle alitangaza wazi hali yake kama hatua ya kutaka watu wenye hali hiyo kukubaliwa na kutonyanyapaliwa katika jamii.

Huyo sio Mbunge wa kwanza kufanya hivyo, Chris Smith wa chama cha Labour alikuwa wa kwanza kutangaza mnamo 2005 kuwa alikuwa akiishi na virusi vya HIV.
Na Fatma Pembe.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KUFUATIA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI - MWANASIASA AJITANGAZA HADHARANI NI MUATHIRIKA KUFUATIA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI - MWANASIASA AJITANGAZA  HADHARANI NI MUATHIRIKA Reviewed by By News Reporter on 12/01/2018 08:52:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.