Loading...
Waziri wa Elimu mafunzo na amali Riziki Juma Pembe alisema Wizara haitomuonea haya kwa yeyote atakaegundulika kuhusika iwe kuchangia au kusababisha mitihani kuvuja sheria itachukua mkondo wake hata awe mtu wa karibu.
Hayo ameyasema huko katika ukumbi wa Mbadala Rahaleo wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa Baraza la mitihani kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhusu kuvuja kwa mitihani na kukiri kuwa mitihani mengine itafanywa hapo tarehe itapotangazwa.
Aidha alisema tumeakhirisha kwa sababu tungeendelea nayo tungefanya maamuzi siyo ya haki kwa walokuwa hawakupata tusingeliwatendea haki.
Alisema iwapo atagundulika mtu yeyote hata awe na ukaribu wa aina gani gani Wizara haitoweza kumvumilia hatua za sheria za utumishi zitachukuliwa ili iwe fundisho kwa wengine na tukio hili lisiweze kutokea tena.
Aliwaomba watendaji wote kuwa na ushirikiano ili ziondoke athari zilizojitokeza , pia suala la uzembe kama hili lisitokee tena watendaji wajiamini kwani walijikubalisha na walikula kiapo hivyo waache tamaa na wawe waadilifu hata Mwenyezi Mungu anahimiza uadilifu.
"Naomba mashirikiano katika utendaji mzima wa kazi ili uzembe huu usitokee tena kwani kila mtu alikula kiapo katika utendaji wake wa kazi muhali uondoke tutakwenda sambamba na nitakula nae sahani moja," Alisema Waziri huyo.
Na Hatibu Kambi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

'OLE WAKE ATAKAYE HUSIKA KUVUJISHA MITIHANI' - WAZIRI ZANZIBAR
Reviewed by By News Reporter
on
12/05/2018 08:32:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: