Loading...

TAHADHARI: WANASAYANSI WAONYA VIRUSI HATARI VYA SAMAKI HUENDA VIKAKUMBA ZIWA VICTORIA

Loading...
Wanasayansi wameripoti kuwa huenda mlipuko wa virusi vya Tilapia Lake Virus, (TilV) vikakumba Ziwa Victoria na hivyo washirika wa ziwa hilo wanapaswa kutoa tahadhari kwa wananchi dhidi ya kula samaki aina ya Sato.

Ripoti hizi zinatokea siku chache tu baada ya Virusi hivyo kugunduliwa nchini Misri.

Virusi hivyo ambavyo havina tiba kwa samaki, vinasemekana kugunduliwa kwa mara ya kwanza Barani Asia katika nchi ya Israel mwaka wa 2009.

Aidha, wanasayansi wanadai kuwa virusi hivyo havina madhara kwa afya ya binadamu lakini kufariki kwa samaki kutokana na virusi hivyo kunazua wasiwasi kuhusu usalama wa chakula na lishe bora.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TAHADHARI: WANASAYANSI WAONYA VIRUSI HATARI VYA SAMAKI HUENDA VIKAKUMBA ZIWA VICTORIA TAHADHARI: WANASAYANSI WAONYA VIRUSI HATARI VYA SAMAKI HUENDA VIKAKUMBA ZIWA VICTORIA Reviewed by By News Reporter on 12/05/2018 09:14:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.