Loading...

MWANAMKE ASIMULIA ALIVYOLAZIMISHWA KUWANYONYESHA NYOKA

Loading...
Mwanamke huyo aliwaacha Wakenya vinywa wazi baada ya kusimulia wazi jinsi mumewe alivyomlazimisha kuwanyonyesha nyoka watatu wa mamake.

Aidha alieleza kuwa familia ya mumewe huyo wa zamani ilikuwa ikiwafuga nyoka wengi nyumbani kwao wanaotumika katika shughuli za ushirikina.

Katika mahojiano ya moja kwa moja katika kituo cha Radio Jambo, alisimulia jinsi alivyoona vioja ukweni kwa mara ya kwanza na alivyoambia kuwa atarajie mgeni.

"Nilipofika nyumbani kwao kwa mara ya kwanza niliambiwa kuwa wageni watakuja na kuwa wakiwasili nisikimbie. Nilikimya maana sikujua kuwa wegeni hao wangekuwa nyoka watatu," alisimulia kwa masikitiko." 

"Mmoja alienda nyuma yangu huku mwengine akilinyonya titi langu. Haya yakiendelea, mtoto wangu alikuwa akinyonya vile vile. Nilifanikiwa kuondoka katika nyumba hiyo," aliongezea.

Akiendelea kusimulia alisema: "Nilikutana na mume wangu Bungoma. Mbali na kuwa mchawi, alitelekeza majukumu yake kama mume," aliongezea.

Mwanamke huyo alieleza kuwa nyoka hao walitumika kuwaua watu waliotoa siri kuhusu kazi yao ya ushirikina. Alieleza kuwa hadi wakati huo, nyoka hao walikuwa wamewaua zaidi ya watu 24.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MWANAMKE ASIMULIA ALIVYOLAZIMISHWA KUWANYONYESHA NYOKA MWANAMKE ASIMULIA ALIVYOLAZIMISHWA KUWANYONYESHA NYOKA Reviewed by By News Reporter on 12/05/2018 10:02:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.