Loading...

TAMASHA LA TIGO FIESTA 2018 KUFANYIKA KABLA YA MWAKA KUISHA

Loading...
MKURUGENZI Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga, kupitia kipindi cha Clouds 360 leo,  amedhibitisha taarifa  za kurudiwa kwa tamasha la Tigo Fiesta kabla ya mwaka huu kuisha.

Kusaga ameyasema hayo wakati wa kuadhimisha mwaka wa 19  tangu kuanzishwa kwa Clouds Media Group.

Tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam lilitakiwa kufanyika Novemba 24, 2018 lakini halikufanyika na sababu ya msingi haikutajwa zaidi ya viongozi kusema kuwa tatizo hilo lilikuwa nje ya uwezo wao.

Alichokisema Joseph Kusaga:
"TIGO FIESTA 2018 lazima ifanyike kabla mwaka kuisha, nimezungumza hadi na Mheshimiwa Rais Dkt Magufuli kwamba pengine suala ni venue,  hili jambo limepenyezwa kwa viongozi wa serikali tumekaa tumezungumza."
Na Asha Lukanda.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TAMASHA LA TIGO FIESTA 2018 KUFANYIKA KABLA YA MWAKA KUISHA TAMASHA LA TIGO FIESTA 2018 KUFANYIKA KABLA YA MWAKA KUISHA Reviewed by By News Reporter on 12/04/2018 04:34:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.