Loading...

ZARI AWAJIBU WALIOSEMA ANANG'ANG'ANIA NYUMBA YA DIAMOND

Loading...
MFANYABIASHARA Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye pia ni mzazi mwenzie na Diamond Platnumz amejikiuta akishindwa kuvumilia maoni ya mashabiki wake mtandaoni wanaomtaka aondoke kwenye nyumba ya kifahari ya mzazi mwenzie, Diamond Platnumz.

Zari kupitia ukurasa wake wa Intagram amesema kuwa hawezi kutoka kwenye nyumba hiyo, kwani yeye na watoto wake (Tiffah na Nillan) walinunuliwa nyumba hiyo ya kuishi.

Mrembo huyo kutoka Uganda ambaye makazi yake kwa sasa yapo Afrika Kusini, amesema kuwa kung’ang’ania kwake sio kwamba hana nyumba nyingine hapana anamiliki nyumba nne Afrika Kusini, bali anaishi kwenye nyumba hiyo kwani ni ya kwake na watoto wake.

Diamond na Zari wameachana mapema mwaka huu baada ya kuishi kwa takribani miaka mitatu kwenye mahusiano, wamefanikiwa kupata watoto wawili Tiffah ambaye ndio mtoto wa kwanza wa Diamond na Nillan.
Na Warrid Julius.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ZARI AWAJIBU WALIOSEMA ANANG'ANG'ANIA NYUMBA YA DIAMOND ZARI AWAJIBU WALIOSEMA ANANG'ANG'ANIA NYUMBA YA DIAMOND Reviewed by By News Reporter on 12/02/2018 07:31:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.