Loading...

MAAJABU YA JUISI YA UBUYU NA FAIDA ZAKE KIAFYA

Loading...
Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

Maajabu ya juisi ya Ubuyu:
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa. 

Zifuatazo ni faida za unga na juisi ya ubuyu kiafya:-

- Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
- Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
- Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
- Ina virutubisho vya kulinda mwili
- Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni muhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
- Inaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
- Huongeza nuru ya macho
- Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
- Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
- Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

Jinsi ya kuandaa juisi yake:
Chukuwa unga wa ubuyu, weka kwenye kikombe, ongeza maji na ukoroge vizuri, unaweza kuongeza sukari au asali, tikisa na unywe.
Na Frank Riziki.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAAJABU YA JUISI YA UBUYU NA FAIDA ZAKE KIAFYA MAAJABU YA JUISI YA UBUYU NA FAIDA ZAKE KIAFYA Reviewed by By News Reporter on 6/30/2019 06:25:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.