Loading...

DEMBELE 'TUMBO JOTO' TETESI ZA NEYMAR KURUDI BARCA

Loading...
Katika klabu ya Bercelona kama kuna mtu anayeombea mabaya dili la Neymar lisikamilike basi ni fowadi wa Kifaransa, Ousmane Dembele.

Ripoti za kutoka Nou Camp zinadai kwamba Dembele hapendezwi kabisa na ripoti za kumhusisha Neymar kurudi kwenye kikosi hicho kwa sababu kutamharibia maisha yake.

Kutokana na hilo, Dembele alikatiza likizo yake kurudi mazoezini mapema ili kuhakikisha anajiweka fiti kumshawishi kocha Ernesto Valverde ili asifikirie kumweka benchi hata kama Neymar atarejea kwenye kikosi hicho.

Dembele amekuwa na wasiwasi baada ya Barcelona kuamua kumsajili staa Antoine Griezmann kwa ada ya Euro 120 milioni kutoka Atletico Madrid jambo linalomtia wasiwasi juu ya nafasi yake kwenye timu kama Neymar naye akitua.

Taarifa zimekuwa hazikauki kuhusu Neymar kuhusishwa na mpango wa kurudi Nou Camp akitokea PSG na kwamba habari hizo zinamkasirisha Dembele.

Siku za karibuni Neymar amekuwa akihusishwa pia na Real Madrid jambo ambalo bila ya shaka litamfanya Dembele kuwa na furaha kama Mbrazili huyo atakwenda kujiunga na wababe wa Bernabeu.
Na Christian Kumalo.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DEMBELE 'TUMBO JOTO' TETESI ZA NEYMAR KURUDI BARCA DEMBELE 'TUMBO JOTO' TETESI ZA NEYMAR KURUDI BARCA Reviewed by GEOFREY MASHEL on 8/11/2019 01:29:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.