Loading...

JE, EID UL-ADHA NI SIKUKUU YA NAMNA GANI?

Loading...
Waumini wa dini ya Kiislamu duniani kote wanasherehekea sikukuu ya Eid ul-Adha. Hii ni moja ya sikukuu za Eid? Baadhi ya watu, hasa wasio waumini wa dini hiyo wamekuwa wakishindwa kutofautisha kati ya Eid ul-Fitr na Eid ul-Adha.

Eid ul-Fitr maana yake ni "sikukuu ya kumaliza mfungo" na kutumiwa kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Siku hii huwa ni siku rasmi ya mapumziko katika mataifa mengi yenye waumini wengi wa Kiislamu. Hata hivyo idadi ya siku za mapumziko huwa tofauti katika nchi mbalimbali.

Waislamu huanza sherehe hizi kwa kukusanyika kwa maombi ya kila mwaka ambayo hufanyika muda mfupi baada ya macheo.

Ni kawaida kuwaona Waislamu wakikusanyika katika misikiti na viwanja vya wazi kwa maoni ya pamoja.

Kabla ya ibada hiyo, huwa wanatoa sadaka kwa maskini (huitwa Zakat) ambayo ni moja ya nguzo kuu katika dini ya Kiislamu.

Ni kawaida kwa miji mikuu mataifa ya Kiislamu kupambwa sana na sherehe kubwa kuandaliwa, watoto kununuliwa nguo mpya na kupewa zawadi mbalimbali.

Siku hii huadhimishwa baada ya kuonekana kwa mwezi wa Shawwal.

Eid ul-Adha:

Eid al-Adha ndiyo sikukuu kuu zaidi ya kidini miongoni mwa Waislamu kote duniani na pia huwa ni siku ya mapumziko mataifa mengi yenye Waislamu.

Nchini Kenya Eid ul-Fitr huwa ni siku ya mapumziko lakini Eid ul-Adha huwa si siku ya mapumziko ya taifa miaka yote, japo mwaka huu hali imekuwa tofauti na leo ni siku ya mapumziko.

Eid al-Adha maana yake ni "sikukuu ya kutoa kafara/kuchinja" kwa Kiarabu na hutumiwa kukumbuka wakati nabii Ibrahimu alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ishmael alivyoamriwa na Allah, lakini akapewa kondoo na Mungu amtoe kafara badala yake.

Sikukuu ya Eid ul-Adha huadhimishwa kuanzia siku ya 10 tangu kuonekana kwa mwezi wa Dhu al-Hijjah.

Ibada ya Hajj kwenda Mecca huanza siku mbili kabla ya Eid al-Adha na tarehe yake huthibitishwa baada ya kuoenakana kwa mwezi huo wa Dhu al-Hijjah.

Eid al-Adha ina majina mbalimbali katika mataifa ya Kiislamu:

- Eid el-Kabir nchini Nigeria na Morocco
- Tabaski nchini Senegal na Gambia.
- Kurban Bayrami nchini Uturuki
- Hari Raya Haji nchini Indonesia, Malaysia na Singapore.
- Eid è Qurbon, nchini Iran.
- Bakr-Id or Qurbani Eid, nchini India, Bangladesh, na kwa Kiurdu pia.

Waislamu pia huvalia mavazi yao mazuri na ya kupendeza siku hii na huenda msikitini kwa maombi.

Baadhi humchinja ng'ombe, mbuzi au kondoo kukumbuka kitendo cha imani cha nabii Ibrahimu.

Hula chakula chenye nyama na huwapa jamaa, majirani na maskini nyama ya mnyama waliyemchinja.

Waislamu hutumia Eid ul-Adha kusherehekea utiifu kamili wa nabii Ibrahimu kwa amri ya Mungu na kuwakumbusha wenyewe kuwa tayari kutoa kafara chochote ili kutimiza maagizo ya Mungu na kumfuata.
Na Hashim Athmani.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JE, EID UL-ADHA NI SIKUKUU YA NAMNA GANI? JE, EID UL-ADHA NI SIKUKUU YA NAMNA GANI? Reviewed by GEOFREY MASHEL on 8/12/2019 08:11:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.