Loading...

RAIS MAGUFULI KUTOA KITITA CHA LAKI 5 KWA KILA MAJERUHI WA AJILI YA MOTO MOROGORO

Loading...
Rais Magufuli ametoa shilingi laki tano kwa kila majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea Morogoro jana alipowatembelea na kuwafariji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 

Rais Magufuli pia ametoa motisha ya fedha kwa wauguzi na madaktari wanaotoa huduma kwa majeruhi hao. 

"Katika taarifa ya Madaktari wamenieleza baadhi ya wengi wameungua nje na ndani sababu ya kuvuta hewa ya Petrol, hawa hawakujitakia hivyo nimeagiza wapate matibabu na chakula kwa gharama zangu nitalipa, Tuvumilie hili linaweza kumpata mtu yeyote, kiukweli hali ni mbaya, lakini tushikamane katika hili, ni majaribu tu ya Shetani na Shetani siku zote anashindwa. " Rais John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli amewahasa wananchi kuto wahukumu waathiriwa kwakuwa hawakujitakia na wangejua hilo wasingefika eneo la tukio.
Na Haika Gabriel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS MAGUFULI KUTOA KITITA CHA LAKI 5 KWA KILA MAJERUHI WA AJILI YA MOTO MOROGORO RAIS MAGUFULI KUTOA KITITA CHA LAKI 5 KWA KILA MAJERUHI WA AJILI YA MOTO MOROGORO Reviewed by GEOFREY MASHEL on 8/12/2019 07:27:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.