Loading...

OMBAOMBA WA USWIZI WAKUMBANA NA SHERIA MPYA, YAWATAKA KUWA NA VIBALI

Loading...
Huko nchini Uswizi katika mji wa Eskilstun imepitishwa sheria inayowataka ombaomba watahitajika kulipia Euro kulipia Euro 21 (sawa na 54,600 pesa Tz) ili waweze kupewa kibali cha kuomba mitaani.

Kwa mujibu wa gazeti la the Guardian, wale wote watakaohitaji kuomba katika mitaa ya mji wa Eskilstun watahitajika kuomba ruhusa ya kufanya shughuli hiyo kwa miezi 3. Atakaye kutwa anaomba bila kuwa na ruhusa hizo atatozwa faini ya Euro 342 (Sawa na Laki 8).

Ombaomba wote watahitajika kuomba kupita Intanet au kituo cha polisi makaratasi ya vibali vya kuwaruhusu kufanya shughuli hiyo ya kuomba mitaani. Sheria hiyo mpya imeanza kutumika mwanzoni mwa mwezi.

Kwa mujibu wa runinga ya taifa ya Uswizi, SVT tangu kuanza kutumika kwa sheria hiyo mpaka hivi sasa ni watu 8 ambao wamekwisha patiwa vibali.
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
OMBAOMBA WA USWIZI WAKUMBANA NA SHERIA MPYA, YAWATAKA KUWA NA VIBALI OMBAOMBA WA USWIZI WAKUMBANA NA SHERIA MPYA, YAWATAKA KUWA NA VIBALI Reviewed by GEOFREY MASHEL on 8/10/2019 06:58:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.