Loading...

RAIS MAGUFULI ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO YA KITAIFA

Loading...
Mhe. Rais Magufuli atangaza siku 3 za Maombolezo ya Kitaifa kuanzia Jumamosi Agosti 10, 2019 kufuatia vifo vya watu zaidi 60 walioungua moto wakati wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika baada ya lori la mafuta kupinduka jirani na kituo kikuu cha mabasi cha Msamvu Mjini Morogoro.

Taarifa hiyo kutoka Ikulu ilisoma:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza siku 3 za Maombolezo ya Kitaifa kuanzia leo Jumamosi tarehe 10 Agosti, 2019 kufuatia vifo vya watu zaidi ya 60 vilivyosababishwa na ajali ya kuungua kwa moto wakati wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika baada ya lori la mafuta kupinduka Mjini Morogoro.

Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 2 asubuhi ambapo lori lenye shehena ya mafuta ya petroli limepindukajirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu Mjini Morogoro wakati dereva alipokuwa akijaribubu kumkwepa mwendesha pikipiki. 

Pamoja na zaidi ya watu 60 kufariki dunia watu wengine takribani 70 wamejeruhiwa na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro na Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Magufuli amemtuma Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kumwakilisha katika mazishi ya Marehemu wa ajali hiyo yanayotarajiwa kuanza kesho Junapili tarehe 11 Agosti, 2019. 

Katika kipindi cha maombolezo bendera zote zitapeperushwa usu mlingoti.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Agosti, 2019

Na Paskali Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS MAGUFULI ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO YA KITAIFA RAIS MAGUFULI ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO YA KITAIFA Reviewed by GEOFREY MASHEL on 8/11/2019 08:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.