Loading...

AJALI MOROGORO: MIILI 21 YATAMBULIWA, SHUGHULI YA MAZISHI KUANZA LEO

Loading...
Morogoro. Serikali kupitia mamlaka za afya imefanya utaambuzi wa vina saba (DNA) kwa miili 21 kati ya 64 iliyotokana na ajali ya moto wa lori lililokuwa limebeba mafuta ya petroli kuanguka na kulipuka eneo la Msamvu mkoani Morogoro.

Sanjari na vifo hivyo, watu 70 waliojeruhiwa, 12 kati yao wamehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kwa matibabu zaidi huku wengine wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.

Hayo yalisemwa jana Jumamosi usiku Agosti 10, 2019 na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,Sera, Bunge,Ajira, Kazi,Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alipozungumza na wanahabari katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

Pia alisema wanaotarajiwa suala la mazishi kwa awamu ya kwanza linaweza kuanza saa 10 jioni leo na  itategemea nafasi ya kutosha ya ndugu kutambua miili ya ndugu zao.

"Kama ndugu atataka kwenda kuzika wenyewe ndugu zao hakutakuwa na shida na tutaanza na Ile miili ambayo inaonyeshwa inashindwa kuhimili na kutaka kuharibika," alisema Mhagama

Alisema miili hiyo itazikwa katika makabuli ya Kila Morogoro na kila mmoja atazikwa kwenye kaburi lake na utaratibu wa majeneza umeandaliwa, sanda na kuchimba makabiri yote na kwamba idadi kamili ya makaburi itaendelea kutokana na mahitaji ya ndugu.

Waziri huyo aliwasihi Watanzania kuendelee kuwa wavumilivu huku akiwataka kuendelea kutoa michango yao ili kukamilisha huduma kwa majeruhi.

Aidha alisema chupa za damu salama 166 zimeshapatikana na misaada ya vitu mchanganyiko mbalimbali imepokelewa yenye thamani ya Sh16 milioni.

Alisema gari lililosababisha ajali tayari limeondolewa eneo la tukio na kutakiwa kusafishwa eneo hilo ambapo mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro amepewa kazi hiyo ili kuwepo na usalama wa watu.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
AJALI MOROGORO: MIILI 21 YATAMBULIWA, SHUGHULI YA MAZISHI KUANZA LEO AJALI MOROGORO: MIILI 21 YATAMBULIWA, SHUGHULI YA MAZISHI KUANZA LEO Reviewed by GEOFREY MASHEL on 8/11/2019 09:37:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.