Loading...
le="text-align: left;">
Mwanamke mmoja mwenye matatizo ya akili alidaiwa kuchomwa moto hadi kufa na vijana wenye hasira kali huko Jimbo la Delta, Nigeria mnamo januari 27 mwaka huu baada ya kukutwa na ya baadhi ya sehemu za mwili wa binadamu kukutwa nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa repoti hiyo, aliwakataza Maafisa wa Usafi walipojaribu kutaka kusafisha kambi yake ya muda iliyopo karibu na makutano ya barabara huko DSC. Wakati akipambana nao kuzuia wasisafishe kambi yake hiyo, vijana wa eneo hilo walimzidi nguvu na hatimaye wakaingia katika kambi aliyokuwa akiishi.
Haraka moja ya kapu lake likafunguliwa katika katika kambi yake hiyo, sehemu za mwili wa binadamu zikaonekana.
Akaanza kupigwa na watu wenye hasira kali na baadaye wakamzungushia matairi na kumchoma na mafuta ya petrol.
MWENDAWAZIMA ACHOMWA MOTO HADI KUFA BAADA YA KUKUTWA NA VIUNGO VYA BINADAMU
Reviewed by By News Reporter
on
1/30/2018 09:50:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: