Loading...
Bw. Dumisani Ngcobo, akiwa ameketi nyumbani kwake. |
Mtu mmoja mkazi wa Pietermaritzburg, Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 43, amesema yeye ni mmoja kati ya wanaume 50 waliokula kichapo na mchungaji wa kanisa kwasababu ni mashoga.
Dumisani Ngcobo ni mwanachama wa kanisa la Shembe Nazareth (eBuhleni). Alisimamishwa uanacha katika kanisa hilo kwa kuwa shoga na kudaiwa alipe faini ya kuiaibisha kanisa.
Ngcobo alisema kuwa imekuwa 'kawaida' kwa mashoga kupigwa kanisani humo. Alisema alikuwa akijiunga katika makambi ya kanisa hilo kila mwisho wa mwaka katika mlima wa Ekhenana huko Tongaat. Wakati wa usiku alipoteza simu yake katika heka heka za kuitafuta akamgusa mmoja wa mwanaume mwenzake.
"Alikuwa amelala pembeni yangu. Wakati natafuta simu yangu nilimgusu. Sikuwa na nia mbaya lakini ilikuwa bahati na akadhani nataka kumfanyia vitendo vya kishoga." Alisema.
Ngcobo alisema aliitwa na mchungajina wazee wa kanisa. "Mhubiri alinionya kwamba kama sitokubali kosa anaweza kuniua. Nilikubali nimemgusa. Nilikuwa naokoa maisha yangu. Nikasema nimemgusa kwa makusudi."
"Baada ya hapo niliitwa kwenye chumba. Mchungaji aliniambia nivue vazi langu la kanisa. Nikajilaza katika kapeti la kanisa. Alichukua fimbo kubwa na kuanza kunichapa. Nilipigwa kuanzia kichwani hadi kwenye miguu. Aliendelea kunichapa mpaka nilipoishiwa nguvu. Nilikuwa mlegevu na mwenye kutokwa na damu kichwani na miguuni. Aliniambia niondoke na kamwe nisirudi tena."
Msemaji wa kanisa Thokozani Mncwabe alisema alitaarifiwa kuhusu kupigwa kwake. Alisema kanisa haliruhusu tabia za ushoga kipindi cha mfungo na maombi. "Sheria ni kwamba mtu yeyote ambaye huenda kinyume na kanuni za kanisa hulipa ada ya uharibifu."
Lakini, alisema, "watu hawapaswi kupigwa. Hiyo ni kinyume na kanisa."
Alipoulizwa kama ni kawaida kwamba mashoga wanapigwa katika kanisa, alisema kuwa "haikubaliki".
Mmoja wa waathirika alithibitisha kuwa huwa wanaume wanapigwa. "Walitumia fimbo. Na tuliperekwa hospitali iliyopo karibu na nyumbani. Familia yangu inalijua hilo lakini wamekaa kimya na kuficha kila kitu. Wanaogopa kuliaibisha kanisa. Lakini tumekuwa kiasi cha kutosha kwa hili. Kuwa mashoga haina maana sisi sio binadamu," alisema mtu ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Ndugu mmoja wa Dumisani Sipho Ngcobo alisema: "Tulishtushwa alipofika nyumbani. Alikuwa akitokwa na damu nyingi kutoka kichwani. Shangazi yangu alimpatia huduma ya kwanza kwa kuzuia damu isitoke na kufunga vidonda.
"Kama kaka yangu ni shoga, kanisa wanapaswa kukemea tabia kama kanisa. Katiba ya Afrika Kusini inaruhusu ushoga. Wanahaki za msingi kama tulizonazo sisi. Kumpiga mtu kwasababu ya jinsia yake ni kosa kisheria."
Sipho Ngcobo alisema kaka yake hakutaka familia ikashtaki polisi. "Tungeshafanya hivyo," alisema.
SHOGA ALA KICHAPO KANISANI
Reviewed by By News Reporter
on
2/01/2018 09:47:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: