Loading...

AFUNGWA JELA KWA KUMSAIDIA MPENZI WAKE KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 13

Loading...
Gemma Hill, mwanamke aliyesaidia ubakaji.
Mwanamke mmoja amefungwa jela kwa kumsaidia mpenzi kumbaka mtoto wa shule wa miaka 13 mara mbili.

Gemma Hill (33), walijadili na mpenzi wake, Stephen Arnopp kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu jinsi watakavyotekeleza ubakaji huo. Mbali na ubakiji huo wa mtoto wa shule wa miaka 13, tayari walishapanga kutekeleza ubakaji wa mtoto wa miaka 9.
Bwana Arnopp, Mbakaji.
Arnopp alishafungwa miaka 11 jela kwa kumbaka binti wa miaka 13 mara mbili mfululizo katika jiji la Welwyn Garden City, Hertfordshire na chupi ya binti huyo ilikutwa nyumbani kwake. Hill yeye, alifungwa miaka sita kwa sababu alimwambia binti huyo asiripoti tukio hilo polisi. Ijapokuwa mtoto huyo aliwaambia walimu na mamlaka zikataarifiwa, na hatimaye wakakamatwa na polisi.
AFUNGWA JELA KWA KUMSAIDIA MPENZI WAKE KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 13 AFUNGWA JELA KWA KUMSAIDIA MPENZI WAKE KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 13 Reviewed by By News Reporter on 2/09/2018 09:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.