Loading...

KAMA UNATAKA KUFANIKIWA LAZIMA UTHUBUTU - Na Siri ya Utajiri

Loading...
Mkufunzi mmoja wa wanyama alimfunga mtoto wa TEMBO kamba mguuni ili asiende mbali na eneo alilomuweka, kamba ile ilikuwa ni ndogo sana lakini kwa tembo huyu mchanga alikuwa bado hana  uwezo wa kuikata kila alipojaribu kufanya hivyo. Ilifika wakati akaamini kuwa hana kabisa uwezo wa kukata kamba ile.

Hata baada ya kuwa MKUBWA bado aliendelea KUAMINI kuwa hawezi kukata kamba ile.  Imani hii ilimfanya asithubutu kufanya jaribio lolote la kukata ile kamba. Aliendelea kubaki sehemu  alipofungwa muda wote pamoja na kwamba kiuhalisia alikuwa na UWEZO wa kuikata kamba ile mara moja na kuondoka.

Katika maisha watu wengi wako kama tembo huyu, kuna vitu wameaminishwa toka wakiwa WATOTO kuwa hawana UWEZO wa kuvifanya, hadi leo bado wanaamini. Hawataki hata kuthubutu KUJARIBU kuona kama inawezekana. Hili limegharimu wengi mafanikio yao.

KUNA KAMBA YOYOTE UMEFUNGWA NA UMEBAKI UKIAMINI KWAMBA HUWEZI KUIKATA? Leo hebu jaribu kusogeza mguu uone kama haiwezi kukatika. 

You Deserve The Best!
Vicent Stephen
KAMA UNATAKA KUFANIKIWA LAZIMA UTHUBUTU - Na Siri ya Utajiri KAMA UNATAKA KUFANIKIWA LAZIMA UTHUBUTU - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 2/09/2018 08:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.