Loading...
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa amesema aliondoka nchini mara tu alipojiuzulu kwenye siasa kutokana na sababu za usalama wake mwenyewe.
Kwa kipindi cha miaka miwili, Dkt. Slaa pamoja na familia yake alikuwa akiishi nchini Canada ambapo alikuwa akifanya kazi katika Supermarket.
Akizungumza na kipindi cha 360 katika Televisheni ya Clouds, Dkt. Slaa alisema alitambua kung'atuka kwake katika siasa kipindi cha uchaguzi kuliongeza maadui wengi kwake ambao ni hatari kwa usalama wa maisha yake.
"Nilienda Canada kwakuwa ni nchi salama ambapo watu wanaishi kwa amani na upendo. Nilijisikia mwenye furaha na amani zaidi," aliongezea "Nilikuwa na maadui kadhaa lakini mara tu baada ya kuondoka upinzani. Ikumbwe pia nilipokonywa ulinzi," alielezea.
Dkt. SLAA: NILIHAMA TANZANIA KWA SABABU ZA KIUSALAMA
Reviewed by By News Reporter
on
2/07/2018 08:26:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: