Loading...
Wanamgambo wa Al Shabaab waliodai kujiunga Al-Qaeda, wakiwa katika shuguli ya kusafirisha mkaa kwenda ASIA. |
Kamanda Mkuu wa Jeshi la nchi ya Somalia, Colonel Aden Rufle amedai wanamgambo wa Al-Qaeda wamejiunga na Al Shabaab na kutengeneza pesa nyingi kupitia biashara ya mkaa.
Akizungumza na kituo cha Redio cha Shabelle kwa njia ya simu, Rufle alisema kwamba anaushahidi wa kutosha kwa madai yake, akiongezea kwamba Al Shabaab wanashirikiana na Jabbaland na wameungana kwa pamoja kusafirisha mkaa kupitia bandari ya Kismayo.
Alisema kuwa boti ndogo zilizobeba mkaa zimepaki bandarini hapo.
Mwaka jana, ripoti ya Umoja wa Mataifa ilionyesha kwamba wanamgambo hao wametengeneza kiasi cha dola za kimarekani milioni 10 kwa mwaka mzima, kupitia biashara ya mkaa wanayosafirisha kuelekea Bara la Asia kupitia Bandari ya Kismayo.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa pia inasema biashara hiyo inawasaidia wanamgambo wa Al Shabaab kuwawezesha pesa kwa ajili ya kuendesha shuguli zao za kigaidi Somalia na nchi za Pwani ya Afrika ya Mashariki.
AL SHABAAB WAJITAJIRISHA KUPITIA BIASHARA YA MKAA
Reviewed by By News Reporter
on
2/07/2018 09:26:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: