Loading...

FAHAMU MAMBO 10 UNAYOPASWA KUFANYA KUPUNGUZA HATARI YA KUUGUA SARATANI

Loading...
Madaktari
Shirika la afya duniani WHO linasema saratani ndio chanzo cha kifo cha mtu mmoja kati ya sita duniani, na hadi 50% ya aina zote za saratani zinaweza kuzuilika.

Lakini idadi ya visa vipya vya ugonjwa huo inatarajiwa kuongezeka kwa takriban asilimia sabiini katika miongo miwili ijayo.

Utumiaji tumbaku ndio hatari kuu ya chanzo cha kuugua saratani na ndio chanzo cha takriban 22% ya vifo jumla vinavyotokana na saratani.

Saratani ya matiti inaongezeka, hususan katika mataifa yanayoendelea, ambapo visa vingi hutambuliwa katika awamu ya mwisho wakati ugonjwa tayari umesambaa mwilini mwa muathiriwa.

Mambo kumi unayoweza kufanya kupunguza hatari ya kuugua saratani:
1.Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote
2. Hakikisha nyumbani kwako hamna moshi
3. Kula chakula chenye afya
4. Kunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani
5. Hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV
6. Epuka kuchomwa sana na miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo.
7. Punguza uchafuzi wa hewa ndani na nje ya nyumba
8. Jishughulishe kuupa mwili mazoezi
9. Punguza unywaji wa pombe
10. Jitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani.
FAHAMU MAMBO 10 UNAYOPASWA KUFANYA KUPUNGUZA HATARI YA KUUGUA SARATANI FAHAMU MAMBO 10 UNAYOPASWA KUFANYA KUPUNGUZA HATARI YA KUUGUA SARATANI Reviewed by By News Reporter on 2/05/2018 06:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.