Loading...
Roy, Baunsa aliyehusika na kifo cha msanii Mowzey Radio. |
Baada kumpumzisha mwimbaji Mowzey Radio katika makazi yake ya milele huko Nakawuka Kanga, karibu na Barabara ya Ntebbe, waombolezaji wenye hasira kali hawakusubiri hata dakika moja na kuamua kwenda katika nyumba ya baunsa huyo wa De Bar baada ya mazishi na kuvamia.
Ni usiku minne iliyopita, Radio alipofikishwa katika kitengo cha Uangalizi wa Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Kliniki ya Case huko mjini Kampala karibu na barabara ya Rubaga baada ya kupata majereha makubwa katika ubongo kutoka na shambulizi alilofanyiwa baa ya De Bar na baunsa aliyejaribu kumtetea bosi wake, pia mmiliki wa baa hiyo amekimbia.
Vyombo vya habari baadaye viligundua kwamba Radio alipata majeraha katika kichwa chake na hata kupoteza fahamu kabla ya umauti kumfika Februari 1 lakini baada ya kumzika waombolezi wenye hasira kali na majozi walivamia na kufanya uharibifu katika nyumba ya baunsa aliyehusika na kifo cha Radio kwa kuona kama ndio njia ya kupata haki yao.
Kwa mujibu wa vyanzo fulani, Roy alikuwa huko huko Dubai miaka kadhaa nyuma na alifukuzwa na kurudi nchini Uganda, na kuanza kufanya mazoezi ya misuli mpaka alipopata kazi katika baa ya De Bar. Hivi sasa ametoroko na hakuna anayejua alipo mpaka sasa lakini polisi bado wanafanya uchunguzi.
JINSI NYUMBA YA BAUNSA ROY ILIVYO HARIBIWA NA WAOMBOLEZAJI
WAOMBOLEZAJI WAVAMIA NYUMBA YA BAUNSA ALIYEHUSIKA NA KIFO CHA MSANII MOWZEY RADIO
Reviewed by By News Reporter
on
2/04/2018 10:06:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: