Loading...

HABARI ZA HIVI PUNDE: WATU 71 WAFARIKI DUNIA KWA AJILI YA NDEGE NCHINI URUSI

Loading...
Ndege ikionekana imeanguaka baada ya kupotea katika dira ya viwanja vya ndege mjini Moscow.
Ndege ya Urusi iliyokuwa imebeba abiria 71 na mhudumu imeanguka baada ya kupoteza mawasiliano ilipokuwa ikiondoka uwanja wa mjini moscow.

Ndege hiyo ya shirika la Saratov ya An-148, ilikuwa safarini kwenda mji wa Orsk wakati ilipoteza mawasiliano.

Huduma za dharura ziliambia vyombo vya habari kuwa ndege hiyo ilianguka na hakuna uwezekano wa kuwapata manusura, dakika kadhaa ikaripotiwa kuonekana lakini hakuna aliyepona.

Inaripotiwa kuanguka karibu na Argunovo kilomita 80 kusini mashariki mwa Moscow.
Kulingana na shirika lingine na habari ndege hiyo ilipotea kutoka mitambo ya rada dakika mbili baada ya kuondoka uwanja wa Domodedovo.
HABARI ZA HIVI PUNDE: WATU 71 WAFARIKI DUNIA KWA AJILI YA NDEGE NCHINI URUSI HABARI ZA HIVI PUNDE: WATU 71 WAFARIKI DUNIA KWA AJILI YA NDEGE NCHINI URUSI Reviewed by By News Reporter on 2/11/2018 05:25:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.