Loading...

KIM JONG-UN AWEKEWA MASHARTI NA RAIS WA KOREA KUSINI

Loading...
Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.
Waziri mkuu wa Korea kusini Lee Nak-yeon amebaini wazi kwamba kuna masharti ambayo lazima yabainishwe kabla ya kukubali mwaliko wa uongozi wa nchi hiyo kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong-un.

Jana katika hatua kubwa ya kidiplomasia kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, alimwalika mwenzake wa kusini kwa mkutano lakini Rais Moon Jae-in bado hajatoa jibu la kuitikia wito huo au la.

Ujumbe huo umetolewa na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un ambaye aliandamana na maafisa wa ngazi za juu zaidi wa Korea Kaskazini kuwahi kuzuru Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea miaka 60 iliyopita.

Hata hivyo hatua hiyo haijafurahiwa na Marekani ambayo ingali inataka kwanza Korea kaskazini ishinikizwe kuachana na miradi yake ya nyuklia.
KIM JONG-UN AWEKEWA MASHARTI NA RAIS WA KOREA KUSINI KIM JONG-UN AWEKEWA MASHARTI NA RAIS WA KOREA KUSINI Reviewed by By News Reporter on 2/11/2018 05:50:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.