Loading...
PENZI LA DHATI
Wanaume si kwamba wanaonyesha kuwa wao hawajatulia kwa kuwatokea wake za watu. Baadhi yao penzi la dhati walilonalo dhidi ya wale ambao wameshaingia kwenye ndoa ndilo huwasukuma kufanya hivyo.
Wanachokifanya wao ni kueleza hisia zao bila kujali kuwa, mlengwa ana mtu au laa. Ndiyo maana mtu huyo anaweza kuwa anajua ukweli kwamba fulani ni mke wa mtu lakini kwa kuwa anaamini huyo ndiye wake, analazimika kujaribu zali.
Siyo dhambi kueleza hisia zako lakini kama unajua kabisa huyo uliyempenda yuko ndani ya ndoa yake au ana mpenzi wake, pambana na hisia zako. Jizuie kwani kumpa usumbufu mke wa mtu ni kujitafutia matatizo bure.
HAKUNA GHARAMA
Baadhi ya wanaume wanawatokea wake za watu kwa kuwa hawatapata usumbufu wa pesa za matumizi, vocha, mavazi na vitu vingine. Wao wanaamini watakuwa wanatoa penzi tu lakini mambo mengine mwenye mke atahudumia.
Lakini wengine wanataka kuanzisha uhusiano na wake za watu kimaslahi. Kwamba mwanaume anaweza kuona mwanamke flani ameolewa na mwanaume mwenye nazo lakini mke anaonekana kutopata penzi analolihitaji. Yeye anatupa ndoano, akiamini akimridhisha kimapenzi, atakuwa anahongwa yeye na maisha yake yatakuwa poa.
USUMBUFU HAKUNA
Kuna wanaume ambao hawapendi kusumbuliwa kwa mambo ya wivuwivu na wapenzi wao, mara nyingi mwanaume anapoanzisha uhusiano na mtu ambaye ana mtu wake anahisi hatasumbuliwa.
Yale mambo ya; ‘uko wapi baby’, uko na nani, nataka tuonane leo’ yanakuwa si kwa kiwango kile ambacho kinakuwepo kwa mtu ambaye hana mtu.
HAKUNA KUGANDANA
Wapo wanaume ambao wao wanataka kila mwanamke mzuri bila kujali ameolewa au yuko singo. Lakini pia wapo ambao hawataki kuingia kwenye uhusiano na mwanamke ambaye atagusia maisha ya baadae. Kwa kifupi wanaume wa staili hii wanaamini wakiwa na wake za watu, hawawezi kugandwa wala kuulizwa juu ya ‘future’.
SIFA TU
Kama ulikuwa hujui wapo wanaume ambao wakitembea na mke wa mtu wanaona sifa sana. Akimtongoza mke wa mtu, akakubaliwa, roho yake inakuwa fresh. Na wengine hawawezi kubaki na siri, kila atakayekutana naye atamwambia; ‘yule mbona nishampitia’.
Hiyo yote sifa. Mtu yuko tayari kutumia gharama yoyote ili mradi atembee na mke/ mpenzi wa mtu, aandike historia kwamba fulani licha ya kwamba ni mke wa mtu lakini ameshatembea naye.
Tuma neno 'MAPENZI' kwenda +255765112259 kupata habari za mahusiano punde zinapojiri.
ZIJUE SABABU KUU ZA WANAUME KUPENDA WAKE ZA WATU
Reviewed by By News Reporter
on
2/28/2018 12:08:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: