Loading...

JACOB ZUMA KONG'OLEWA LEO KATIKA KITI CHA URAIS?

Loading...
Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini.
Kufuatiwa na kashfa inayomkabili rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma kwa kutumia vibaya pesa za serikali ya nchi hiyo chama chake cha ANC kimeweka ngumu kwamba endapo watabaini na kwamba taarifa hizo ni za kweli basi atapaswa kuachia ngazi katika ki cha urais mapema kadri itakavyowezekana.
Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma.
Akizungumza kaika mkutano wa hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu.
Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa hilo angekitaka.
Bwana Ramaphosa alikuwa akizungumza katika kumbukumbu ya miaka 28 toka Rais wa kwanza mzalendo nnchini humo Nelson Mandela alipolihutubia taifa, mara tu baada ya kuachiwa gerezani.
JACOB ZUMA KONG'OLEWA LEO KATIKA KITI CHA URAIS? JACOB ZUMA KONG'OLEWA LEO KATIKA KITI CHA URAIS? Reviewed by By News Reporter on 2/12/2018 10:39:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.