Loading...

MAREKANI: TUPO TAYARI KUFANYA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI

Loading...
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence amesema kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini bila ya kuwepo masharti yoyote.

Katika kile kinachoonekana kama kubadilika kwa msimamo wa Marekani, Bw Pence aliliambia gazeti la the Washington Post kuwa ikiwa Korea Kaskazini inataka mazungumzo, basi utawala wa Trump utafanya hivyo.

Lakini amesisitiza kuwa vikwazo vitakuwepo hadi Korea Kaskazini ichukue hatua za kumaliza mpango wake wa silaha za nyuklia.

Bw Pence alikuwa akizungumza akiwa njiani kutoka kwa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi nchini Korea Kusini, ambapo alifanya mazungumzo na Rais Moon Jae-in.

Utawala wa Trump awali ulisema kuwa hautafanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon-un ikiwa tu yuko tayari kuachana na mpango wa nyuklia.
MAREKANI: TUPO TAYARI KUFANYA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI MAREKANI: TUPO TAYARI KUFANYA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI Reviewed by By News Reporter on 2/12/2018 11:07:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.