Loading...
Tumbili akijaribu kumpanda Paa. |
Serikali ya kaunti ya Muranga imeshutumiwa kwa kutenga fedha za kukabiliana na tumbili wavamizi katika kijiji cha Gatunyu huko Gatanga.
Kaunti hiyo imetangaza vita vikali dhidi ya wanyama hao na imeanza mpango kwa jina 'Tafuta Tumbili' kuwakabili wanyama hao.
Lakini huku wakulima hao wakiwa na matumaini kwamba sasa wataweza kuvuna mazao yao baada ya wanyama hao kukamatwa, baadhi ya wakaazi katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakilidharau wazo hilo.
Katika mtandao wa kijamii Peter Kamau alielezea hatua hiyo ya serikali ya kaunti kuwa ya majuto wakidai kuwa ni njia ya utumizi mbaya wa fedha kwa kuwa haikujadiliwa na bunge la kaunti.
''Serikali ya kaunti inapaswa kujua kwamba licha ya kilimo kugatuliwa inafaa kuweka muda wao mwingi katika kukamilisha mradi wa kiwanda cha maziwa na kuwacha jukumu la kukabiliana na wanyama kwa wataalamu wa shirika la wanyama pori la KWS'', alisema Kamau.
Zaidi ya tumbili 10,000 wanalengwa katika mradi huo ambao utaendelea hadi mwezi Machi 24 kufuatia ombi la wakulima kwa kaunti hiyo wakilalamikia uharibifu wa chakula na nyasi za mifugo unaotekelezwa na wanyama hao.
Operesheni hiyo ilianza siku ya Jumamosi mjini Gatanga ambapo takriban tumbili 125 walikamatwa kupitia mitego na wengine kuuawa.
Serikali hiyo ya kaunti imetoa nambari ya simu kwa wakaazi wa kaunti hiyo ili kuwasaidia kuwakamata tumbili hao.
Tumbili hao waliodaiwa kupelekwa katika msitu jirani na watu wasiojulikana miaka kadhaa iliopita wamekuwa wakiharibu mimea mbali na kuwanyanyasa wanawake na watoto.
Anastasia Mugure , mkaazi wa kijiji cha Ngangaini village, anasema kuwa wanawake wanalazimishwa kutembea na silaha ili kujitetea iwapo watashambuliwa na wanyama hao.
''Hawaogopi hata kuingia jikoni na kuchukua chakula kutoka kwa sufuria hadi pale kunapokuwa na mwanamume kwa nyumba'' , alisema akiongeze kwamba wanalazimika kununua chakula baada ya wanyama hao kuharibu mimea yao kwa misimu miwili mfululizo''.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
KENYA: WAKULIMA WATANGAZA VITA DHIDI YA TUMBILI
Reviewed by By News Reporter
on
2/22/2018 12:28:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: