Loading...
Mkutano wa wafadhili wa kikosi cha ukanda cha G5 Sahel ulifanyika siku ya Ijumaa, Februari 23 katika majengo ya Tume ya Ulaya mjini Brussels, nchini Ubelgiji.
Viongozi wa nchi zaidi ya thelathini za Ulaya walihudhuria mkutano huo pamoja na marais wa tano wa nchi za ukanda wa Sahel.
Washirika wapya kama vile Uturuki, au Afrika Kusini pia waliwakilishwa na mawaziri wao wa kigeni. Lengo la mkutano huu ni kutafuta fedha zaidi kwa ajili ya kufadhili mwaka wa kwanza wa operesheni ya kikosi hiki cha pamoja kitakachopambana dhidi ya Boko haramu na makundi mengine ya kigaidi katika ukanda huo.
Mkutano huo ulijadili jinsi ya kupata zaidi ya euro milioni 300 ya bajeti iliyotengwa kwa kikosi hiki cha G5 Sahel. Kwa sasa inaonekana kuwa ni vigumu kupatikana kwa kiwango hiki, kwani tayari Umoja wa Ulaya ulikubali kutoa euro milioni 50, huku kikosi hiki kikiwa tayari kimekusanya euro milioni 250. Pamoja na nchi arobaini zitakazowakilishwa katika mkutano huo, waandaaji wa mkutano wana imani kuwa watafikia haraka malengo yao.
Malengo ambayo yanaonekana ni tofauti kwa kila upande. Nchi za ukanda wa Sahel zinabaini kwamba kikosi cha G5 Sahel kinahitaji euro milioni 423 ili kuanza operesheni yake. Hoja ambayo haiungwi mkono na Ufaransa. "Pamoja na milioni 300, kikosi hiki kina uwezo wa kuendesha operesheni zake za kwanza," Ikulu ya Elysee imebaini.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
KIKOSI CHA 'G5 SAHEL' KINACHOANDALIWA KUPAMBANA NA BOKO HARAMU CHAZIDI KUPATA UFADHILI
Reviewed by By News Reporter
on
2/27/2018 11:00:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: