Loading...

DADA WA KIM JONG-UN AWASILI KOREA YA KUSINI KATIKA MASHINDANO YA OLYMPIC

Loading...
Dada yake rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.
Dada yake Kim Jong-un rais wa Korea Kaskazini amekuwa wa kwanza katika familia yao kufika katika ufunguzi wa mashindano ya Winter Olympic nchini Korea Kusini.

Yeye ndio mtu wa kwanza katika familia ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kukanyaga katika mashindano kwa miaka 60 iliyopita tangu vita ya Korea 1950 - 1953 ambayo iliigawa nchi ya Korea.

Kim Yo Jong, mwenye miaka 30, aliwasili Korea Kusini kwa ndege binafasi ya kaka yake kama ni sehemu kubwa ya kuheshimu ufunguzi wa mashindano hayo ya Pyeongchang Winter Olympics. Na atakuwepo nchini humu kwa siku tatu ndipo atarejea Korea Kaskazini.

Wakiwa pamoja na Waziri wa Burudani Kim Jong Nam wamepanga kukutana na rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in Jumamosi ya leo Ikulu. Moon anajaribu kutumia fursa ya michezo kama fursa ya kudumisha mawasiliano mazuri kati yake na Korea Kaskazini.
DADA WA KIM JONG-UN AWASILI KOREA YA KUSINI KATIKA MASHINDANO YA OLYMPIC DADA WA KIM JONG-UN AWASILI KOREA YA KUSINI KATIKA MASHINDANO YA OLYMPIC Reviewed by By News Reporter on 2/10/2018 05:52:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.