Loading...

RAPPA TYGA AMEDAI KUWA MTOTO WA KYLIE JENNER NI WAKE NA KUTAKA VIPIMO VYA 'DNA'

Loading...
Tyga ameripotiwa akitaka vipimo vya vinasaba (DNA) vya mtoto wa Kylie Jenner akiamini kwamba stormi ni mwanae.

Kylie Jenner amekuwa mama kwa kipindi cha wiki moja lakini tayari kumetokea utata wa nani ni baba wa mtoto wake.

Kwa mujibu wa mtandao wa Radar Online, aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Kylie Jenner ametaka vipimo vya DNA kwakuwa anadhani stormi ni mtoto wake bila ya kupingwa na mtu yeyote.

Chanzo kinadai kwamba Kylie na Tyga walikuwa bado wapo katika mahusiano miezi 9 kabla ya kuzaliwa kwa mtoto stormi, ingawa walivunja mahusiano yao kabisa Aprili 2017.

Pia Tyga alidiriki kuwaambia hadi marafiki zake kwamba bado wanashiriki kimapenzi na Kylie Jenner  miezi 9 iliyopita, wakati mimba ndio inatungwa.

Na amesema anamaswali mengi sana yanayohitaji majibu kuhusu mtoto stormi, ikiwa anahitaji sana kukutana na mtoto na kupata ufafanuzi juu uhalali wa umiliki wa mtoto huyo.
RAPPA TYGA AMEDAI KUWA MTOTO WA KYLIE JENNER NI WAKE NA KUTAKA VIPIMO VYA 'DNA' RAPPA TYGA AMEDAI KUWA MTOTO WA KYLIE JENNER NI WAKE NA KUTAKA VIPIMO VYA 'DNA' Reviewed by By News Reporter on 2/10/2018 04:30:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.