Loading...
Waziri mwenye dhamana ya kusimamia mwongozo wa taifa na maswala ya kidini nchini Zambia Bi. Godfridah Sumahili ameibuka na kusema serikali haitoruhusu matumizi ya midoli ya mapenzi, ambayo inaonekana kushika kwa kasi katika nchi za Afrika.
Kwa mujibu wa waziri Godfridah, amedai Zambai itasimamia misingi yake ya maadili ili kulinda wananchi wake kuathirika na uteja wa matumizi ya midoli ya mapenzi.
Aliendelea kusema: "Vitabu vya mungu vinasema mwili wa mwanaume ni mali ya mwanamke, na mwili wa mwanamke ni mali ya mwanaume".
Waziri huyo mwenye dhamana aliyasema hayo baada ya nchi za Afrika ya Kusini kutangaza kuwa vitetemeshi na midoli ya mapenzi haviruhusiwi na ni kosa kisheria ukikutwa navyo.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, Esther Katongo, amedai sheria ya nchi ya Zambia inachukulia kufanya biashara, kutumia au kununua midoli ya mapenzi ni kosa la jinai.
Mtandao wa Mwebantu News Portal umeripoti kuwa wananchi wengi wameunga mkono kauli aliyozungumza waziri kwa kupiga vita matumizi ya midoli ya mapenzi na vifaa vingine vya ngono.
Wakati biashara hii ya midoli ya mapenzi ikizidi kupamba moto duniani, watengenezaji wa midoli hiyo wamesema jamii inatafsiri vibaya maudhui ya teknolojia yao kwa sababu wao walikuwa na lengo la kutatua matatizo ya ukahaba na watu wanaoishi peke yao.
KIMBUNGA CHA MIDOLI YA MAPENZI YAIKUMBA ZAMBIA
Reviewed by By News Reporter
on
2/08/2018 02:12:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: