Loading...

ANUSURIKA KUKATWA UUME KISA WIVU WA MAPENZI

Loading...
Lusaka, Zambia mwanaume mmoja kwa kijina, Namakando Sitali (29) anusurika kukatwa uume wake na mkewe, Elizabeth Phiri (23) kwa madai ya kumsaliti mkewe kwa kumjaza mimba mwanamke mwingine nje ya ndoa.

Wawili hao walioana mwaka 2016, na wamebahatika kupata mtoto mmoja. Phiri mkewake alisema: "Tuliishi kwa furaha katika ndoa yetu kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka nilipogundua mume wangu amempa ujauzito mwanamke mwingine nje na kuanza kumpigia simu kuhusu maendeleo ya uja uzito huo."

Aliendelea kusema: "Sitali alianza kunipiga nilipomuuliza kuhusu huyo mwanamke na kunilaza na njaa bila kunipa pesa ya chakula," aliongezea "Sitali alikuwa anawaambia rafiki zake waje kutazama televisheni nyumbani kwetu mpaka saa 5 usiku wakati bado yupo kazini."

Phiri aliendelea kusema zaidi: "Wakati mwingine Sitali alinipiga na alichukia sana nilipomuuliza alikuwa wapi usiku kucha."

Kwa mujibu wa mtandao wa ZambiaObserver, kwa maswahibu yote hayo aliyoyapata mwanamke huyo, aliamua kujaribu kukata uume wa mwanaume wake ili atulie kwakuwa aliamini ndio kitu pekee kinachomfanya mumewe Sitali asitulie nyumbani na ugomvi unaotokea kila siku.

Lakini tukio hilo lilisabisha kuperekana mahakamani na hata kutengana.
ANUSURIKA KUKATWA UUME KISA WIVU WA MAPENZI ANUSURIKA KUKATWA UUME KISA WIVU WA MAPENZI Reviewed by By News Reporter on 2/08/2018 12:52:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.