Loading...

DAVID BECKHAM AZINDUA KAMPENI YA KUTOKOMEZA MALARIA

Loading...
Mchezaji David Beckham, akifurahi na watoto.
Kampeni mpya duniani ya kuangamiza ugonjwa wa malaria - 'Malaria Lazima Ife ili Mamilioni Waweze Kuishi' - Imezinduliwa kupitia tovuti na mitandao ya kijamii. Kampeni hiyo inaongozwa na Mashirika ya Kimataifa ya Afya na Maendeleo, ikiwemo shirika la Malaria No More, na idadi kadhaa ya watu maarufu.

Kampeni ilizunduliwa kwa kipande cha video cha mchezaji nguli David Beckham, akionekana katika boksi la vioo 'akizungukwa' na mbu wenye njaa kali. Kampeni hiyo mwanzo ililenga nchi za Jumuia ya Commonwealth ambapo nusu ya vifo vya malaria vinapatikana huko lakini baadae inatarajiwa kugusa duniani kote.

"Hawa wadudu hawaishi sehemu kama U.K. lakini sehemu nyingi duniani uking'atwa na mbu inaogopesha na inaua," alisema Beckham.

Ingawa mafanikio yameonekana kwa miaka ya karibuni, lakini malaria imeendelea kuua watu 445,000 kwa mwaka.

"Hii haikubaliki kabisa," alisema Beckham, mwanachama na kiongozi wa Baraza la Malaria No More na Balozi wa hiari wa UNICEF.
DAVID BECKHAM AZINDUA KAMPENI YA KUTOKOMEZA MALARIA DAVID BECKHAM AZINDUA KAMPENI YA KUTOKOMEZA MALARIA Reviewed by By News Reporter on 2/08/2018 11:56:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.