Loading...
Mipira hiyo mipya ya kike inayosemekana inaladha murua ishaanza kujaribiwa huko nchini Uganda.
Wataalam wanasema inampa ladha mwanamke na kumpa nguvu ya maamuzi wakati wa tendo. Mipira hiyo ya kuvaa kama chupi imesharuhusiwa na Baraza la Sayansi na Teknolojia nchini Uganda ili ianze kutumika katika matumizi ya banadamu.
Mipira hiyo mipya ni muunganiko wa Lingerie na Contaceptive iliotengenezwa kwa kutumia polyurethane na kukusidiwa kutumiwa mara kwa tendo. Na imetengenezwa kwa utando mwembamba sana, hata kumfanya mtumiaji hasihisi kama anatumia mpira, alisema Dkt. Moses Muwonge, Mkurugenzi wa SAMASHA Medical Foundation, watangazaji wa mipira hiyo.
Mipira hiyo imetengenezwa nchini Colombia na kampuni ya Innova Quality na inatarajiwa kuingia sokoni rasmi mwezi Oktoba, kwa mujibu wa Muwonge. Na wanatarajia kuisambaza kote Afrika ili Waafrika waweze kunufaika na ugunduzi wa mipira hiyo uliofanyika Chuoni Makelele miezi sita iliyopita.
Pia unaweza ukuivaa kutwa nzima kama chupi ila ukaitumia pale tu utakapohitaji kufanya tendo, alisema Dkt. Muwonge akielezea jinsi inavyotumiwa.
'CONDOM ZA CHUPI' ZA KIKE ZAZINDULIWA NCHINI UGANDA
Reviewed by By News Reporter
on
2/08/2018 11:04:00 AM
Rating:
Tanzania zipo
JibuFuta